Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 April 2015
Wednesday, April 08, 2015

Yanga ni chereko-chereko, yazidi kujitupa kileleni.


Na George Mganga
Yanga Afrika imezidi kuonesha ubora wake jioni ya leo ikithibitisha kuwa haikuwatoa BDF na Platinum Fc kwa kubahatisha mara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa goli 8-0 dhidi ya Coast Union kutoka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ushindi huo sasa umeiwezesha Yanga kufikisha points 43 na hii ni mara baada ya kucheza michezo 20 huku Azam Fc ikiwa inafuatia ikiwa imecheza michezo 19 na sare ya bao 1-1 leo inawafanya wafikishe pointi 37.
Mliberia Kpah Sherman ambaye toka ang'ae wakati anaingia nchini kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe II na baada ya hapa kutokuwa na mwenendo mzuri ndani ya timu hiyo leo imekuwa kama ameondoa nuksi baada ya kutoa nafasi 3 za magoli na alifanikiwa kufunga goli moja pia dakika ya 50.
Amis Tambwe leo amekuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga mara baada ya kutia goli 4 kibindoni peke yake ikiwa ni zaidi ya Hat trick na kujibebea kubeba mpira mara baada ya mchezo huo, Tambwe alifanikiwa kufunga magoli yake dakika ya 10, 33, 47 na 90.
Magoli mengine yalifungwa na Saimoni Msuva dakika ya 24 na 68 ambaye bado anajikita katika kwenye namba moja katika orodha ya wafungaji hadi sasa akiwa na goli 13 halikadhalika Salum Telela naye alifunga dakika ya 89.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Edward Charles dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga dk67, Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Kpah Sherman/Nizar Khalfan dk70 na Simon Msuva.
Coastal Union; Bakari Fikirini, Juma Hamad, Abdallah Mfuko, Yussuf Chuma, Bakari Mtama, Abdulhalim Humud, Mohamed Ally, Yahya Ayoub, Rajab Mohamed/Mohammed Shekuwe dk57, Ike Bright Obinna/Mohamed Mtindi dk64 na Rama Salim/Abbas Athuman dk46.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!