Na George Mganga
Ratiba ya mechi za kwenda kushiriki michuano ya AFCON mwaka 2017 imepangwa leo huku Tanzania ikiwa imepangwa katika kundi G pamoja na wababe ikiwemo mafarao wa Misri halikadhalika Nigeria na Chad katika fainali ambazo zitafanyika huko Gabon.
Droo hiyo imefanyika leo mjini Cairo, Misri huku Gabon ikifanikiwa kuzipiku Ghana na Nigeria kuwa mwenyeji mshirika wa michuano hiyo ya AFCON itakayokuwa ya 31.
Mwaka 2012 Gabon walikuwa washirika wenyeji wa michuano hiyo halikadhalika wenyeji wao Equatorial Guinea.
Makundi ya kufuzu AFCON 2017 yapo hivi;
Kundi A; Tunisia, Togo, Liberia na Djibouti.
Kundi B; DRC, Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Madagascar.
Kundi C; Mali, Equatorial Guinea, Benin na Sudan Kusini.
Kundi D lina timu za Burkina Faso, Uganda, Botswana na Comoros.
Kundi E; Zambia Kongo, Kenya na Guinea Bissau.
Kundi F, Cape Verde, Morocco, Libya na Sao Tome.
Kundi G; Nigeria, Misri, Tanzania na Chad.
Kundi H; Ghana, Msumbiji, Rwanda na Mauritius.
Kundi I; Ivory Coast, Sudan, Sierra
Leone na Gabon.
Kundi J; Algeria, Ethiopia, Lesotho na Shelisheli.
0 comments:
Post a Comment