Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 April 2015
Thursday, April 09, 2015

Barcelona waanza kumnyemelea Matteo Darmian


Na George Mganga
Mkurugenzi wa timu ya Torino Giogio Parinetti amekuwa akizungumzia mara kwa mara malengo na matarajio ya wachezaji wa kilabu yake wanaocheza nafasi ya beki ikiwemo na Matteo Darmian pamoja na beki mwingine wa kati Kanil Glik.
Wachezaji hawa wawili wamekuwa wakifuatilia na vilabu vikubwa barani huyu huku Fc. Barcelona wakimlenga zaidi Matteo Darmian jambo ambalo limemfanya Mkurugenzi wa timu hiyo kuliweka wazi.
"Kuwa na wachezaji kama Damian na Gilk ni hatua ya kwanza na ni nzuri katika kuijenga timu.
"Tunajua itakuwa ni vigumu sana tukiwang'ang'ania kutokana na idadi ya vilabu ambavyo kimekuwa vikiwahitaji na kuwaulizia" Peritti alisema wakati anazungumza na jarida la Tuttorsport.
Matteo Darmian (25) alitokea katika kilabu akademi ya Ac. Milan na alivutiwa kuingia Torino misimu miwili iliyopita japo haikuwezekana kutokana na kuitwa kutumikia Taifa lake katika fainali za kombe la Dunia zilizofanyika huko Brazil mwaka jana.
Ukweli ni kwamba Barcelona kwasasa hairuhusiwi tena kufanya usajili hadi itapofikia mwaka 2016 na kama wanauhitaji naye wanaweza kumsainisha January.
Ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kucheza nafasi tofauti tofauti upande wa beki, kulia kushoto mara nyingi anatumia nafasi hizo.
Turink mara nyingi hutumia mabeki watatu wa nyuma ili kuamsha mashambulizi vizuri kwenda mbele.
Kama Barcelona wakimchukua kijana huyo anaweza akawa mbadala mzuribwa Dan Alves ambaye yupo katika mikakati ya kuondoka hapo Barcelona wakiwa wote wanacheza nafasi sawia.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!