Na George Mganga
0688665508
Kilabu ya Yanga ipo katika mkakati maalumu wa kuvunja akaunti yao ya benki ili kumrejesha kundini aliyekuwa mchezaji wao, Didier Kavumbagu kabla hajaenda Azam Fc na kufunga mabao 10 msimu huu.
Kavumbagu ambaye yupo na klabu ya Azam Fc hivi sasa akiwa anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya mwaka huu, ametajwa na Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuph Manji kuwa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kurejeshwa kikosini hapo.
Wakati Kavumbagu anachukuliwa na Azam, kiungo Frank Domayo naye akachukuliwa na wanalamba lamba hao matukio yaliyoleta taharuki kubwa kwa wapenzi na wanachama wa Yanga huku wakionyesha kuchukizwa sana na wakaushutumu uongozi kwa uzembe wao.
Kwa mujibu wa gazeti la Dimba linasema kuwa kwa habari ambazo limezipata kutoka kwa kigogo mmoja wa kamati ya usajili ya Yanga zinasema kuwa wamekabidhiwa jukumu la kuhakikisha wanamny'akua mapema mchezaji huyo kabla hajaongeza mkataba mpya na Azam Fc.
Kigogo huyo tayari ameshaanza usiri wa mazungumzo na mchezaji huyo wa Azam ambaye hadi hivi sasa anashikilia nafasi ya pili ya ufungaji wa magoli akiwa na goli 10 huku Msuva wa Yanga akiwa na goli 11 ambaye ndiyo anaongoza.
Dimba alifanikiwa kumtafuta Afisa habari wa Yanga Jerry Murro kuzungumzia suala hilo lakini hakuwa tayari kusema lolote na kudai kwasasa wapo katika maandalizi ya kombe la Shirikisho.
Yanga itakutana na Etou du Sahel katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Africa mara baada ya kuitupia virago BDF na Fc Platinum.
0 comments:
Post a Comment