Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 April 2015
Tuesday, April 07, 2015

Meck Mexime awatuliza mashabiki wa timu yake.


Na George Mganga
Kocha mkuu wa timu ya Mtibwa Sukari iliyopo mjini Morogoro amesema kwamba anahitaji uvumilivu na utulivu kwa mashabiki wa timu hiyo akiwa na imani kubwa ya kikosi hicho kusimama tena kama awali.
Akizungumza na waandishi wa habari kocha huyo amesema kuwa wamekuwa hawafanyi vizuri siku za usoni na hivyo kusababisha baadhi ya mechi mfululizo kupoteza hali ambayo imekuwa ikishangaza japo ndivyo matokeo ya mpira yanavyokuwa.
"Kila kitu chetu kipo vizuri, tunafanya mazoezi vizuri na mambo yote yapo vizuri japo kile kinachotokea mbele yetu kimekuwa kinamshangaza kila mmoja wetu.
"Tunachokiangalia kwasasa mbeleni ni kuhakikisha tunashinda na kupata pointi tatu (3) kwa kila mechi tutayocheza ambazo zimesalia" alisema Mexime.
Mtibwa Sukari hadi sasa ipo nafasi ya 12 na ikiwa na pointi 23 kibindoni ligi kuu Tanzania Bara na hii ni mara baada ya kupoteza katika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga dhidi ya Stand United.
Kumbuka Mtibwa Sukari ilifanikiwa kumaliza raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara ikiwa imeshinda mechi 8 bila kupoteza na ikiwa namba 1 kileleni mwa ligi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!