Na George Mganga
Akiwa kama kocha wa Simba Sports Club kwa wakati huo, Moses Basena sasa amepata kibarua cha kuinoa kilabu ya Simba ya Uganda mara baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu bila timu ya kufundisha
Basena ambaye aliondoka katika klabu ya Simba msimu uliopita akiwa kama mkurugenzi wa benchi la ufundi, sasa amepata kibarua hicho huku akiwa na ndoto ya kukifikisha mbali zaidi kikosi hicho alichojiunga nacho.
Mtu wa karibu wa Kocha huyo alilidokeza kuwa wamekubaliana kumsainisha ndani ya timu hiyo mara baada ya kuona CV zake zinakubalika na sasa yupo tayari kuibeba mikoba na kuanza kusaka pointi tatu kila ashukapo dimbani.
"Bassena anafundisha Simba ya hapa Uganda mara baada ya kuachana na Ukurugenzi wa timu ya Simba ya Dar es salaam mwaka uliopita" chanzo hicho kilinena.
"Ni timu ambayo inashiriki ligi kuu nchini hapa japo ilipoteza umaarufu siku za hivi karibuni" kiliendelea chanzo hicho toka Uganda kutupa taarifa.
0 comments:
Post a Comment