Na George Mganga
Bingwa mtetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Azam Fc leo ameshindwa kufurukuta mbele ya Wanazambarau kutoka Mbeya, Mbeya City baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi jijini Dar es salaam.
Mara baada ya mchezo huo Azam sasa wamefikisha pointi 37 huku wakiwa wanaweka utofauti wa pointi 6 na Yanga ambayo ndiyo inaongoza ligi hadi sasa ikiwa imefikisha point 43 mara baada ya ushindi wa leo dhidi ya Coast Union wa goli 8-0.
Katika mchezo huo Azam ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika goli kupitia kwa mchezaji Kipre Michael Balou mnamo dakika ya 61 kwa shuti kali ambalo lilichukua umbali wa takribani mita 25 na kushinda golikipa wa Mbeya City.
Mapema tu dakika kadhaa mbele Mbeya City waliweza kusawazisha goli hilo kwa njia ya penati mara baada ya mchezaji wao Deus Kaseke kufanyiwa madhambi katika eneo ka hatari na penati hiyo ikifungwa na Rafael Daud Alpha dakika ya 64.
Baada ya mchezo huo kuwa 1-1 dakika zilizobakia timu hizo zilikuwa zikishambuliana zamu kwa zamu kila moja ikiwa inajitahidi kupata goli ila mwisho wa siku hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Azam 1-1 Yanga.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Serge Wawa, Mudathir Yahaya, Himid Mao, Kipre Bolou/Gaudence Mwaikimba dk80, Frank Domayo/Amri Kiemba dk56, John Bocco na Brian Majwega/Farid Mussa dk74.
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, Peter Richard, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso,
Christian Sembuli, Kenny Ally, Deus Kaseke/ Hamad Kibopile dk84, Paul Nonga/Peter Mapunda dk70, Raphael Alpha, Themi Felix na
Peter Mwilanzi.
0 comments:
Post a Comment