Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 April 2015
Saturday, April 25, 2015

Okwi kuendeleza makali yake leo?




Na George Mganga



Timu kongwe nchini Tanzania klabu ya Simba SC inatarajia kushuka dimbani jioni hii  katika uwanja wa Taifa kumenyana na timu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara katika muendelezo wa michezo ya mwisho mwisho wa msimu huu.

Katika mchezo huo simba wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Mgambo JKT walioupata siku ya jumatano katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo uliopita ulishuhudiwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi akiwa katika kiwango bora na kufanikiwa kufunga magoli matatu"Hat trick" huku lingine likifungwa na Ramadhani Singano"Messi".


Ukiitazama Simba iliyocheza na Mbeya City na Simba iliyocheza juzi dhidi ya Mgambo JKT ni timu ambayo kwa kiasi kikubwa ilionekana kubadilika mara baada ya wachezaji wake muhimu kurejea katika kikosi cha kwanza.

Okwi alitengeneza kombinesheni nzuri na viungo wenzake hali iliyoifanya timu hiyo ambayo bado ina ndoto ya kushika nafasi ya pili kuwa nzuri. Mechi na Mbeya City Okwi aliikosa mechi hiyo baada ya kuwa na kadi tatu za njano.

Lakini Ndanda FC wanaoshikiria nafasi ya 8 wakiwa na pointi 28 bado wanahitaji sana pointi tatu kujihakikishia kutokushuka daraja.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!