Na George Mganga
Kocha mkuu wa Arsenal maarufu kama "The Gunners" Arsene Wenger, amesema kuwa ujio wa aliyekuwa golikipa wa Chelsea, Peter Cech (33) na sasa amesajiliwa Arsenal anaweza kuwa Edwin Van der Sar wa baadaye.
Cech anafananishwa na kipa huyo ambaye alifanikiwa kutwaa mataji 11 katika kipindi cha miaka minne toka ajiunge na mashetani wenye makazi yao mjini Manchester.
Kipa huyo ambaye alisajiliwa tokea Chelsea ambapo alikipiga katika dimba la Stamford Bridge kwa ada ya paund milioni 11 mapema mwezi wa 6 mwaka huu alifanikiwa kutwaa mataji 15 ikiwemo kombe la ligi kuu mara (4) na moja la UEFA.
Van der Sar alijiunga na Manchester United mnamo mwaka 2005 wakati akiwa na miaka 34 huku akifanikiwa kutwaa kombe la UEFA mara moja pamoja na mataji ya ligi kuu ya Uingereza kwa miaka tofauti.
Licha ya kutwaa mataji 11 akiwa na Manchester United, Van de Sar aliweza kutundika daruga na mashetani hao ilipofikia mwaka 2011.
Wenger anasema Van der Sar alikuwa na Man United kwa takribani miaka sita akitokea katika klabu ya Fulham kwa maana hiyo haoni sababu ya Cech kukosa ubora kama wa kipa huyo kwa miaka atakayotumika timu ya Arsenal.
"Ni mchezaji mzuri mwenye bidii na juhudi awapo mazoezini na uwanjani, ana nidhamu pia hulifanya goli lionekane dogo awapo langoni.
"Ni mtu ambaye yupo makini, hana matatizo, anaonekana kama mchezaji aliyejengwa kucheza mpira wa Kiingereza zaidi, nadhani ni kipa mwenye ueledi zaidi" alisema Wenger.
Wenger aligundua Cech kuwa ni kipa mzuri hata kabla hajajiunga na timu ya darajani, Chelsea wakati huo ikiwa na mwaka 2004 japo hakufanikiwa kumpata baada ya Jose Mourinho kumpiga kwata kwenye usajili huo.
0 comments:
Post a Comment