Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 August 2015
Saturday, August 01, 2015

Remy aweka nia ya kukamia nyavu msimu mpya.

Na George Mganga
Mshambuliaji wa Chelsea, Loic Remy ameweka nia ya kufanya vyema zaidi msimu ujao wa ligi kuu Uingereza kutokana na kukosa nafasi hiyo msimu uliopita.
Remy ana imani kuwa kuongezeka kwa Radamel Falcao ambaye alisajiliwa kwa mkopo toka As Monaco kuwa sasa atajituma zaidi ili haki ya namba yake itumike vilivyo.
Mchezaji huyo hakuwa na bahati ya kucheza mechi zote msimu ulioisha licha ya kucheza mechi sita tu za mwanzo na baadae alikosa namba kutokana na uwepo wa Didier Drogba na Diego Costa.
Katika msimu uliopita Diego Costa ndiye alikuwa mtu pekee aliyeongoza mstari wa mbele pia Didier Drogba naye alikuwa sehemu ya ushambuliaji katika kikosi hicho.
Hata hivyo ukiachilia mbali mechi sita alizocheza hapo mwanzo, Remy aliweza kuchangia kupata magoli saba ndani ya timu hiyo.
Kocha mkuu wa timu hiyo, Jose Mourinho amesema licha ya kukosekana kwake msimu uliopita, baada ya ujio wa Falcao bado ana imani naye na ataendelea kuwa moja ya Key Players wa kikosi hicho.
"Nataka kuleta kila kitu katika timu yangu, nitajituma japo najua ligi itakuwa ngumu na si kama ya msimu uliopita sababu kila timu zimejiandaa.
"Wachezaji wote wanapaswa kuwa bora zaidi ya walivyokuwa msimu uliopita, tunapaswa kupigana ili tuweze kufunga zaidi" alisema Remy.
Loic ana imani atakuwa mmoja wa wachezaji ambao watajumuishwa katika kikosi ambacho kitacheza na Arsenal (FA Cup Winners) katika Ngao ya Hisani siku ya Jumapili (kesho).

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!