Na George Mganga
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameitaka timu yake kutafuta ushindi wa mapema katika
pambano la mwishoni mwa wiki hii Jumamosi dhidi ya Reading.
Kocha huyo raia wa Ufaransa
amesema kuwa vijana wake wanapaswa kuanza kwa kasi na nguvu katika mchezo huo
utakaopigwa katika dimba la Wembley kama kweli wanahitaji kutetea taji lao.
Wenger amesema kwamba timu yake imejifunza msimu uliopita ambapo walihitaji penati kuishinda
Wigan katika hatua ya nusu fainali kabla ya kutanguliwa goli mbili na wapinzani wao Hull City katika pambano la fainali ambapo hadi mwisho wa kipute hicho, waliibuka kidedea kwa ushindi
wa mabao 3-2.
Mechi hiyo itakuwa ni nusu fainali ya kumi kwa mzee Wenger ,huku akidai kwamba Arsenal inajiamini hasa kutokana na kushinda mechi nane mfululizo.
Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili ambapo Aston Villa itawakaribisha Liverpool.
0 comments:
Post a Comment