Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 April 2015
Tuesday, April 07, 2015

Huu ndiyo usajili kabambe wa Manchester United.


Na George Mganga
Manchester United wanataraji tena kuwa makini sana ifikapo majira ya joto na kutokana na taarifa,inadaiwa huenda wakatumia kiasi cha pauni milioni 105 juu ya kusajili sura tatu mpya.
Mashetani wekundu wapo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kumaliza katika nne bora na kurudi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Louis Van Gaal anataka kuendeleza maendeleo yake ndani ya Old Trafford kwa kufanya mabadiliko kadhaa tena kwenye majira ya joto.
Ndani ya dirisha lake la kwanza la usajili Van Gaal alitumia zaidi ya pauni miloni 150 kwa wachezaji kama Angel Di Maria, Luke Shaw, Daley Blind, Ander Herrera na Marcos Rojo, na yupo tayari kutumia pesa nyingi tena mwaka huu.
Katika rada yake kuna Raheem Sterling kutoka Liverpool, Memphis Depay kutoka PSV na Mats Hummels kutoka Borussia Dortmund.
Inaaminika Sterling atakuwa ghali zaidi,akigharimu kiasi cha pauni milioni 50,wakati Hummels huenda akasainishwa kwa kiasi cha pauni milioni 35 na Depay kununuliwa kwa pauni milioni 20 tu.
Man United watapata upinzani kwa hawa wachezaji kutoka katika klabu kadhaa ikiwemo wapinzani wao wote kwenye Ligi Kuu ya Uingereza ambao wanavutiwa na nyota hao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!