Mourinho ampigia debe John Terry
Na Florence George
Baada ya kucheza kwa kiwango cha juu msimu huu na akiwa tayari ameshaisaidia timu yake kuchukua kombe la LIGI maarufu kama 'Capital One' nahodha wa chelsea John Terry anatarajiwa kupewa mkataba mpya wa kuendelea kukipiga na vijana hao wa darajani.
Akiongelea suala la John Terry kuongezewa mkataba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alisema 'natambua kuwa atakuwa mchezaji wa chelsea msimu ujao'.
Pia aliendelea kusema kuwa 'nafahamu kitu gani bodi yangu imeniambia sina shaka Terry ataenda kupata mkataba wake '.
Terry mwenye umri wa miaka 34 tayari ameshaichezea timu yake zaidi ya michezo 550 tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa mwaka 1998 na inaonekana anaweza kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kama ilivyo kawaida ya sera ya klabu ya Chelsea ya kuongezea miezi 12 kwa wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30.
Terry aliiongoza Chelsea kutwaa ubingwa wa ligi mara mbili katika awamu ya kwanza ya Jose Mourinho kuiongoza timu hiyo kabla ya kuwa katika kipindi kigumu chini ya kocha Rafael Benitez katika msimu wa 2012/2013.
Mpaka sasa Chelsea ndio inaongoza ligi kuu Uingereza ikiwa na pointi 60 katika michezo 26 iliyocheza pointi tano mbele ya Manchester City iliyonafasi ya pili ambayo tayari imeshacheza michezo 27 mpaka sasa.
Chelsea inajiandaa kupambana na West Ham United katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza siku ya jumatano usiku.
0 comments:
Post a Comment