Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 January 2015
Thursday, January 08, 2015

Azam Fc Out Mapinduzi Cup!


Na John Oscar

Michezo ya robo fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea huko visiwani Zanzibar, leo hii katika mchezo wa mapema ilishuhudia bingwa mtetezi KCCA kutoka nchini Uganda  wakiaga michuano hiyo baada ya changamoto ya mikwaju ya Penalty dhidi ya Polis Zanzibar.

Kwa matokeo hayo, Polis Zanzibar wamefuzu kwa hatua ya nusu fainali na watakwenda kupambana na Simba Sc ambao walifuzu baada ya hapo jana kujipatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Taifa Jang'ombe ya huko visiwani Zanzibar.

Mchezo mwingine ni ule ambao uliwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, timu ya Azam Fc dhidi ya vinara wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Mtibwa Sugar ambapo baada ya dakika 90 kumalizika, timu hizo zilikuwa zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.

Katika changamoto ya mikwaju ya Penalty, Azam Fc wameondolewa baada ya Aishi Manula na Kipre Tchetche kupoteza mikwaju yao na kufanya mtibwa kushinda kwa mikwaju 7-6. 

Mtibwa Sugar sasa wanafuzu kwa hatua ya nusu fainali na mshindi baina ya mchezo wa Yanga vs JKU unaopigwa usiku huu, utaamua ni nani atakwenda kumenyana nao kwenye hatua ya nusu Fainali.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!