Borussia Dortmund wamerejea kwenye ubora wao.
Na Florence George
Baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus katikati ya wiki hii ,timu ya Borussia Dortmund imeendeleza ushindi wake wa nne mfululizo baada ya kushinda magoli 3-0 dhidi ya Schakle 04 katika mchezo wa ligi kuu nchini Ujerumani.
Katika mchezo huo mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi na timu ya Schakle 04 Klaas-Jan Huntelaar alirejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu yake huku pia kocha Roberto Di Mateo alimuanzisha goli kipa Timon Wellenreuther mwenye umri wa miak 19.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ndio alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake katika dakika ya 78 kabla ya Henrikh Mkhitaryan kufunga la pil katika dakika ya 79 na Marco Reus akifunga bao la tatu dakika ya 86.
Ushindi huo umefanikiwa kuwapeleka Dortmund hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa na alama 28 na sasa wameanza kuonyesha mwanga wa kupigania moja ya nafasi nne za juu ili kupata nafasi ya kucheza klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment