Rooney amaliza ukame wa magoli.
Na Florence George
Nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney alimaliza ukame wa kutofunga goli katika mechi nane ya ligi kuu nchini Uingereza baada ya hiyo jana kufunga magoli mawili na kuisadia timu yake kuondoka na pointi zote tatu mbele ya Sunderland,mchezo uliochezwa katika dimba la Old Trafford.
Katika mchezo huo ambao vijana wa kocha Louis Van Gaal walitawala kwa asilimia kubwa walianza kupata goli dakika ya 66 kwa njia ya penati iliyofungwa na Rooney, baada ya mchezaji John O'shea kumchezea faulo mshambuliaji wa United Radamel Falcao.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wes Brown alionyeshwa kadi nyekundu badala ya O'shea aliyemchezea faulo Falcao,kabla ya Rooney kuongeza goli la pili dakika ya 84.
Kwa matokeo hayo sasa Manchester United imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 katika michezo 27 iliyocheza msimu huu,pointi mbili zaidi ya Arsenal iliyonafasi ya nne huku ikitarajiwa kumenyana na Everton hii leo pale katika uwanja wa Emirates.
Matokeo mengine,katika mchezo wa mapema hiyo jana West Ham United walikubali kipigo cha magoli 3-1 kutoka kwa Crystal Palace,huku Aston Villa ilifikisha mchezo wa 12 bila ushindi baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United shukrani kwa goli la mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papiss Cisse.
Timu ya Southampton ilifungwa goli 1-0 na timu ya West Bromwich Albion goli lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Burundi Saido Berahino.
Nayo Swansea City walipanda hadi nafasi ya nane baada ya kuifunga timu ya Burnley goli 1-0,pia Stoke city nayo ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Hull City, goli lililofungwa na Peter Crouch.
Mpaka sasa timu ya Chelsea ndio inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 60 katika michezo 26,ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 55 katika michezo 26 pia ,Manchester United ni ya tatu ikiwa na pointi 50 katika michezo 27 huku Arsenal ikikamilisha Top Four ikiwa na pointi 48 imkiwa imeshacheza michezo 26.
0 comments:
Post a Comment