Yanga ni timu isiyoeleweka!
Na Samuel Samuel
Siku moja tulikuwa na rafiki yangu Ibrahim Mlele ndani ya viwanja vya Boko veterans. Ni viwanja ambavyo klabu ya soka ya Yanga ilivitumia kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Simba SC uliopigwa Octoba 18 mwaka Jana.
Wakati mazoezi yakiendelea Ibra aliniuliza swali, " hivi Sam una uhakika Yanga itashinda?" Ilinichukua kama dakika mbili kumjibu. Jibu nililompa lilimkwaza kidogo kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa timu hiyo.
Nilimjibu " inaweza kufungwa au kudroo" mwisho wa siku Yanga walitoka sare ya tasa na Simba ambayo kabla ya mechi ilionekana kama ni dhaifu.
Unajua kwa nini? Klabu ya soka ya Yanga ambayo usiku wa leo itapambana na timu ya Jang'ombe ina tatizo moja kubwa la muda mrefu. Mara nyingi timu hiyo inapoimarika kila idara huwa inajikuta inapoteza michezo rahisi sana.
Wakati mashabiki wa timu hiyo wakiipigia chapuo timu yao kuondoka na ushindi basi hujikuta inafungwa au kutoa droo. Hakuna aliyetegemea Yanga ingepoteza mchezo dhidi ya Mgambo JKT na kujikuta inatema ubingwa.
Inawezekana vipi kuingia akilini beki ya Tshabalala na Isiaka kuwazuia wakongwe kama Niyonzima , Ngasa na Kiberenge Msuva?
Wakati Yanga ikiwa imeandaliwa vizuri chini ya Maximo ilijikuta inapoteza mchezo wa kwanza kwenye ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ilihali mashabiki wake waliipa nafasi kubwa kushinda na kukusanyana kila pembe ya nchi lakini mwisho wa siku wakajikuta wanashangazwa.
Matokeo ya juzi 2-2 dhidi ya Azam FC yaliwaduwaza wengi wakitazama soka safi la vijana hao lakini mwisho wa siku utamaduni ukaendelezwa. Wachezaji wa Yanga ni lazima wajijengee dhana ya kujituma hasa kila mechi ili iache kuwashangaza mashabiki wake.
Ukiwatazama Jang'ombe ni timu inayocheza soka la pasi fupi fupi na kasi ya wastani wakati yanga ya Pluijm iliyocheza na Azam FC inacheza soka hilo hio lakini Yanga wana kasi na nguvu sana. Kama Hans hatotaka kubadirisha kikosi chake basi wana uwezo wa kuibuka washindi.
0 comments:
Post a Comment