Chikoti Cico
Klabu ya West Ham imefanikiwa kuingia raundi ya nne ya kombe la FA baada ya kuitupa nje ya kombe hilo timu ya Everton kwenye mchezo wa marejeano uliopigwa kwenye uwanja wa Boleyn Ground.
Mchezo huo ambao uliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo kuwa sare ya magoli 2-2 kwa dakika zote 130 ambazo zilichezwa, West Ham waliibuka wababe kwa kufunga penati 9 kwa 8 kati ya penati 20 zilizopigwa kwenye mchezo huo.
Kabla ya timu hizo kuingia kwenye hatua ya mikwaju ya Penati magoli ya West Ham kwenye mchezo huo yalifungwa na Valencia kwenye dakika ya 56 na Carlton Cole kwenye dakika 113 huku magoli ya Everton yakifungwa na Mirallas kwenye dakika ya 82 na Lukaku kwenye dakika ya 97.
Kipa wa West Ham, Adrian Castillo aliibuka shujaa kwenye mchezo huo baada ya kuokoa penati mbili za Mirallas na Joel huku akifunga penati ya mwisho na kuipa ushindi timu hiyo inayofundishwa na kocha Sam Allardyce na kwa ushindi huo West Ham itakutana na Bristol City kwenye raundi ya nne ya kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment