Na Chikoti Cico
Mchezaji mahiri wa timu ya Real Madrid Christiano Ronaldo amezawadiwa viatu vilivyonakshiwa kwa almasi na wadhamini wake baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa duniani maarufu kama Ballo d’Or hapo Jumatatu.
Nike ambao ndiyo wadhamini wakuu wa mchezaji huyo wameamua kumtengezea Ronaldo viatu hivyo vipya ikiwa ni kama shukrani kwa mwaka mzuri wa 2014 ambao Ronaldo alishinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya, kombe la Mfalme (Copa del Rey) kombe la UEFA (UEFA Super Cup), Kombe la dunia kwa klabu (Club World Cup) na Ballon d’Or.
Viatu hivyo ambavyo vina rangi ya dhahabu vimenakshiwa kwa almasi kwenye logo ya CR7 ya mchezaji huyo ambayo imeweka katika sehemu ya kisigino cha mguu ya kiatu hicho, logo hiyo ni vifupisho vya majina yake mawili na namba anayoichezea uwanjani.
Ronaldo alinyakua tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2014 hapo Jumatatu kwa kuwashinda Lionel Messi na Manuel Neuer hii ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo na ikiwa ni kwa mara ya tatu kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment