Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2015
Friday, January 30, 2015

Uchambuzi: Manchester United vs Leicester City.


Na Chikoti Cico

Nyasi za uwanja wa Old Trafford zitawaka moto siku ya Jumamosi kuanzia mida ya saa 12 jioni ambapo timu ya Manchester United itaikaribisha Leicester City kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal kwenye mchezo huo atamkosa kiungo Michael Carrick ambaye ana majeraha ya misuli na atakuwa nje kwa wiki karibu nne, pia atamkosa Ashley Young ambaye alikuwa majeruhi ingawa anakaribia kurejea uwanjani huku kiungo Darren Fletcher ambaye uhamisho wake kwenda West Ham ukikaribia kukamilisha akiondolewa kikosini kwenye mchezo huo.
Wakati huo huo mabeki Jonny Evans na Chris Smalling wanatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosekana kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Cambridge kutokana na kuwa majeruhi, wakati huo huo timu ya Manchester United mpaka sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 40.
Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha kiungo wa United Juan Mata amefunga magoli matano katika mashuti saba aliyopiga na kulenga golini kwenye michezo mbaimbali ya ligi kuu nchini Uingereza pia takwimu zinaonyesha kumekuwa na magoli matano katika michezo minne iliyoihusisha United. Kikosi cha kocha Van Gaal kinaweza kuwa hivi: De Gea; Valencia, Jones, Rojo, Shaw, Blind; Mata, Di Maria, Rooney; Van Persie, Falcao
Nayo klabu ya Leicester City inayoshika mkia kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 17 inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kupigana kufa na kupona ili kupata alama tatu muhimu na kujitengenezea mazingira mazuri ya kuondoka kwenye balaa la kushuka daraja.
Kocha wa Leicester City Nigel Pearson kwenye mchezo huo atawakosa Kasper Schmeichel na Chris Wood ambao ni majeruhi pia Matty James atakosena kwenye mchezo huo akitumikia adhabu ya kufungiwa mechi naye Riyad Mahrez hatakuwepo kutokana na majukumu ya timu ya taifa ya Algeria kwenye michuano ya AFCON.
Kikosi Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha klabu ya Leicester City imeshinda mchezo mmoja tu na kufungwa michezo saba huku ikitoka sare mchezo mmoja kati ya michezo tisa iliyopita ya ligi dhidi ya United. Pia takwimu zinaonyesha Leicester imecheza rafu mara 285 mpaka sasa kwenye msimu huu wakizidiwa na Crystal Palace peke yao ambao wamecheza rafu mara 299.
cha kocha Nigel Peasron kinaweza kuwa hivi: Hamer; Simpson, Wasilewski, Morgan, Konchesky; Drinkwater, Cambiasso; Schlupp, Kramaric, Vardy; Ulloa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!