Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Uchambuzi: Everton vs Manchester City SAA 12 JIONI.


Na Chikoti Cico

Nyasi za uwanja wa Goodison Park zitashika moto wikendi hii pale ambapo wenyeji timu ya Everton itakapoialika Manchester City katika moja ya mchezo unaotarajiwa kuvuta hisia za wapenzi wengi wa ligi kuu nchini Uingereza.

Everton ambao wanashika nafasi ya 13 wakiwa na alama 21 kwenye msimamo wa ligi wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu baada ya kupoteza michezo minne iliyopita ya ligi.

Kocha wa Everton Roberto Martinez kwenye mchezo huo dhidi ya Man City atawakosa James McCarthy’s, Sylvain Distin, Tim Howard, Tony Hibbert, Leon Osman, Darron Gibson na Steven Pienaar ambao ni majeruhi.

Huku mabeki Antolin Alcaraz aliyekuwa amepewa adhabu na Leighton Baines ambae alikuwa majeruhi wakitarajiwa kurejea kikosini.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha timu ya Everton imefungwa michezo sita na kushinda mchezo mmoja tu huku ikitoka sare mchezo mmoja katika michezo minane iliyopita ya ligi.

Pia takwimu zinaonyesha kocha wa Everton Roberton Martinez amekuwa na rekodi mbaya dhidi ya City akiwa meneja kwani katika michezo 11 aliyokutana nao amefungwa michezo 10 na kutoka sare mchezo mmoja.

Kikosi cha Everton kinaweza kuwa hivi: Joel; Coleman, Jagielka, Stones, Baines; Barry, Besic, Mirallas, Barkley, Naismith, Lukaku.

Nayo timu ya Manchester City ambayo inaongoza msimamo wa ligi pamoja na Chelsea ikiwa na alama 46 inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kujikita kileleni na kuiacha Chelsea.

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini kuelekea mchezo huo atamkosa kiungo wake mahiri Yaya Toure ambaye ameenda kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika lakini kurejea kwa Sergio Aguero, Edin Dzeko na Vicent Kompany kutakiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo dhidi ya Everton.

Takwimu za Manchester City kuelekea mchezo huo zinaonyesha City hawajafungwa katika michezo 11 iliyopita ya ligi huku wakishinda michezo tisa na kutoa sare michezo miwili naye kiungo wa Man City David Silva takwimu zinaonyesha amefunga magoli matano katika michezo sita iliyopita ya ligi.

Kikosi cha Manchester City kinaweza kuwa hivi: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Clichy; Fernando, Fernandinho; Nasri, Silva, Milner; Jovetic

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!