Na Chikoti Cico
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye hivi karibuni alilalamika kwamba kuna “kampeni ya kichinichini” dhidi ya Chelsea kutoka kwa waamuzi wa ligi kuu nchini Uingereza kauli iliyopelekea kocha huyo kuadhibiwa na chama cha soka cha Uingereza (FA) anakabiliwa na tuhuma nyingine za kumtukana mwamuzi wa mchezo wa Chelsea dhidi ya Spurs.
Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema Mourinho alimtukana mwamuzi Phil Dowd ambaye alichezesha mchezo kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya Chelsea, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa White Hart Lane na Spurs kushinda kwa magoli 5-3.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema Mourinho alimropokea mwamuzi huyo kwa kusema “we ni mnene sana kuwa mwamuzi, ungestaafu, umetugharimu” huku akionyesha kugadhabika na maamuzi ya mwamuzi huyo ambapo aliinyima Chelsea penati wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Ingawa taarifa pia zinasema Mourinho alienda kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Dowd uwanjani White Hart Lane na walizungumza na kuwekana sawa baada ya tukio hilo kutoonekana kwenye taarifa ya mwamuzi huyo.
0 comments:
Post a Comment