Shaqiri azitolea nje timu za Uingereza
Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uswisi Xherdan Shaqiri amefanikiwa kujiunga na timu ya soka ya Inter Milan ya nchini Italia akitokea katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani wiki iliyopita na kufanikiwa kusaini mkataba wa miaka minne ambapo atakuwa katika timu hiyo hadi mwezi June 2019.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akihusishwa na baadhi ya timu za Uingereza ambapo klabu za Liverpool, Everton na Stoke City zilikuwa zinahusishwa na kumuhitaji mchezaji huyo.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kujiunga na timu hiyo siku ya Jumatano, Shaqiri alisema kuwa kulikuwa na ofa mbalimbali kutoka Nchini Uingereza na Ujerumani lakini ndoto yake ilikuwa kucheza katika timu ya Inter Milan.
Aliendelea kusemaJuventus hata ikimuhijati lakini amejiunga na Inter mara baada ya kuongea na kocha wa timu hiyo Roberto Mancini na kumueleza mikakati ya timu hiyo.
Shaqiri alijiunga na timu ya Bayern Munich mwaka 2012 akitokea timu ya Fc Basel ya nchini Uswisi na amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu nchini Ujerumani na kombe moja la klabu bingwa barani Ulaya.
Shaqiri alikuwa hapati namba ya kudumu katika kikosi cha Wajerumani hao ambapo msimu huu amefanikiwa kucheza michezo nane na kufanikiwa kufunga nmagoli matano huku akisaidia upatikanaji wa magoli mengine mawili.
0 comments:
Post a Comment