Na Chikoti Cico
.
Kiungo na nahodha wa timu ya Liverpool, Steven Gerrard ana hatihati ya kukosekana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Capital One dhidi ya Chelsea mchezo utakaochezwa tarehe 20 ya mwezi Januari.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alitolewa baada ya kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland Jumamosi iliyopita ambapo Liverpool walishinda kwa goli 1-0 ili kumlinda na kukaza kwa ukano wa mvungu wa goti (hamstring).
Kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Aston Villa utakaochezwa mwisho wa juma hili bado kuna wasiwasi kama Gerrad atakuwa fiti kucheza mchezo huo na kama hatacheza kuna uwezekanao wa kushindwa pia kucheza masaa 72 baadaye dhidi ya Chelsea.
Gerrard ambaye mwisho wa msimu huu ataiacha klabu ya Liverpool na kujiunga na klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani kuelekea michezo hiyo mwili ya Liverpool dhidi ya Aston Villa na Chelsea ataendelea kufanya kazi na timu ya madaktari wa klabu yake ili kujiweka fiti.

0 comments:
Post a Comment