Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo de Lima anataka kurejea uwanjani kwa mara nyingine tena baada ya kustaafu kwa muda mrefu, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38 anataka kuichezea klabu ya Fort Lauderdale kutoka Amerika ya Kaskazini inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo.
Ronaldo ambaye mara ya mwisho kucheza soka ilikuwa ni mwaka 2011 kwenye klabu ya Corinthias ya nchini Brazili anataka kurejea tena uwanjani lakini ni ikiwa tu kama ataweza kuwa fiti vya kutosha kuweza kuichezea klabu hiyo ya Fort Lauerdale inayoshiriki ligi daraja la pili.
Akiongea na waandishi wa habari mbele ya Meya wa Fort Lauerdale Ronaldo alipoulizwa kama ana mpango wa kurejea uwanjani alisema “hiyo sio rahisi kwasababu napenda kucheza, napenda kucheza soka, hayo yalikuwa maisha yangu yote, mpenzi wangu mkubwa, nilipostaafu, niliacha kucheza kwasababu ya mwili wangu, mauimvu mengi na majeraha”
Kucheza mchezo wa soka unahitaji kuwa fiti, ntajaribu mwenyewe, ni changamoto nyingine. Nina hakika itasaidia ligi na kuisaidia timu. Nitafanya mazoezi sana na kama (kocha) atanihitaji labda” aliongeza huku akitabasamu kwamba atacheza kama washambuliaji watafika fainali.
Ronaldo ambaye aliwahi kuzichezea klabu za PSV Eindhoven, Inter Milan, Barcelona, AC Milan na Real Madrid ataungana na Raul Gonzalez mwenye miaka 37 ambaye walicheza wote Real Madrid ambaye kwasasa anaichezea klabu ya New York Cosmos kwenye ligi hiyo ya Amerika ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment