Na Chikoti Cico
Gwiji wa timu ya taifa ya Colombia, Faustin Asprila amedai uhusiano wa mshambuliaji wa Manchester United Radamel Falcao na kocha Louis van Gaal umevunjika na mchezaji huyo atarejea Monaco baada ya muda wake wa mkopo kuisha mwishoni mwa msimu.
Inasemekana Falcao ambaye alishangazwa baada ya kuachwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kilichoenda kucheza na Southampton siku ya Jumapili baada ya kuanza kwenye michezo mitano iliyopita alizungumza na Van Gaal siku ya Jumatatu mazoezini Carrington kuhusu kuachwa kwenye mchezo huo.
Akiongea na IB Times UK Asprila ambaye aliwahi kuichezea klabu ya Newcastle United alisema “kama Van Gaal akiendelea (Falcao) ataondoka nadhani ni uhusiano ambao tayari umeshavunjika, Falcao anaelewa kwamba kocha hamuhitaji.
Nakumbuka wakati nilipoenda Newcastle Kevin Keegan alinihitaji, aliniunga mkono sana na hapa ni wazi kwamba Van Gaal hamuamini Falcao”
“Ni huzuni kuona jinsi anavyomfanya Falcao, tatizo sio Falcao ila kocha. Falcao alikuwa na majeraha mapema kwenye msimu lakini baada ya kuthibitisha kamba bado ni mfungaji kama alivyokuwa alicheza michezo mitano na kufunga magoli.
Aliendelea kusema “lakini hii yote ni kuhusu kumwamini, baada ya kucheza vizuri kwa michezo kadhaa haieleweki kwamba ghafla ameacha kucheza.
Ukweli ni kwamba sijui ni nini Van Gaal anajaribu kufanya pale United na nadhani wachezaji pamoja na mashabiki pia wamechanganyikiwa anafanya mabadiliko mengi bila sababu”.
0 comments:
Post a Comment