Arsenal vs Hull City :Emirates saa 2:30 Usiku
Na Oscar Oscar Jr
Leo ni kama marudio ya Finali ya kombe la FA iliyopigwa msimu uliopita pale Wembley ambapo timu ya Arsenal itawaalika Hull City kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe hilo uliyopangwa kufanyika majira ya saa 2:30 ndani ya dimba la Emirates.
Tayari kuna mabadiliko kuelekea mchezo huo ambapo kwa upande wa Arsenal, mchezo huo unaweza ukamshuhudia mshambuliaji Theo Walcott akirejea kwenye kikosi cha kwanza.
Golikipa David Ospina anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Wojciech Szczesny ambaye hakuwa na kiwango kizuri kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Southampton ambapo timu hiyo ilipoteza kwa kuchapwa bao 2-0.
Kwa upande wa Hull City wao watanufaika na kurejea kwa Tom Huddlestone na Stephen Quinn ambao walikuwa wamefungiwa huku kocha Steve Bruce akiendelea kuwakosa Andrew Robertson, Liam Rosenior na Gaston Ramirez ambao walipata maumivu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya timu ya Everton.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa na kurudisha kumbukumbu ya fainali ya msimu uliopita ambapo Arsenal walifanikiwa kutoka nyuma kwa bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo kwa bao 3-2 na kuwaacha Hull City hawaamini kilichotokea.
Arsenal Wenger ameendelea kujiamini licha ya kikosi chake kutoaminika na hii ni kwa sababu kocha huyo wa Kifaransa ameshatwaa taji hilo mara tano akiwa na Arsenal.
Akizungumza kuelekea mchezo huo ameweka wazi kuwa lengo lao ni kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo na kuhakikisha wanapambana kutetea ubingwa huo.
0 comments:
Post a Comment