Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 January 2015
Saturday, January 10, 2015

Mario Manduzkic kutua Arsenal.


Na Oscar Oscar Jr

Habari zilizotoka leo kwenye magazeti ya Uingereza, zimemuhusisha mshambulia wa kimataifa wa Croatia na klabu ya Atletico Madrid, Mario Manduzkic kuwa njiani kujiunga na timu ya Arsenal.

Manduzkic alinunuliwa na mabingwa hao wa Hispania kabla ya kuanza kwa msimu huu akitokea klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani na lengo ilikuwa kuje kuziba nafasi ya Diego Costa aliyekwenda kwenye klabu ya Chelsea.

Manduzkic ambaye tayari amefunga mabao sita kwenye La Liga tangu alipojiunga na Atletico, imelezwa kuwa hana furaha kwenye klabu hiyo kutokana na kukosolewa kila siku anapokosa magoli na baadhi ya mashabiki na wana habari.

Ujio mshambuliaji Fernando Torres hivi karibuni kwenye klabu hiyo akitokea Ac Millan, umeongeza uwezekano wa mchezaji huyo kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza na njia sahihi anaona ni kuondoka.

Kwa mujibu wa gazeti la Metro, Arsenal tayari wameshapelea ombi rasmi la kunyakuwa mchezaji huyo. Kama Arsenal watampata, utakuwa ni msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Alexies Sanchez, Olivier Giroud na Danny Welbeck.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!