Gonzalo Higuain kutua Liverpool
Na Oscar Oscar Jr
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina na klabu ya Napoli, Gonzalo Higuain ameingia kwenye rada za Liverpool na sasa kocha Brendani Rodgers ametajwa kumfukuzia kwa karibu mshambuliaji huyo ili kuhakikisha anatua Anfield kabla ya dirisha hili la usajili la majira ya baridi kufungwa.
Taarifa zilizotoka leo kwenye magazeti ya nchini Italia, imesemekana tayari kocha wa Napoli, Rafael Benitez amekamilisha usajili wa mshambuliaji, Manolo Gabbiadini kutoka klabu ya Sampdoria kwa Pauni 11M na hii ni ishara kuwa kuna uwezekano mkubwa Higuain kutua Liverpool.
Liverpool wamekuwa katika mawindo ya kupata mshambuliaji ambaye atakuja kuongeza nguvu na kuziba pengo lililoachwa na Luiz Suarez aliyetimkia klabu ya Barcelona na majeruhi ambayo yamekuwa yakimuandama Daniel Sturridge ambaye kwa sasa ameonekana kurejea tena dimbani.
Higuain ambaye hapo awali alikuwa na klabu ya Real Madrid, endapo uhamisho wake utakamilika na kujiunga na Liverpool kuna uwezekano mkubwa wa kuiongezea makali liverpool katika jitihada zao za kutaka kumaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment