Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

Chelsea angalau wamejipoza machungu.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuchapwa mabao 5-3 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tottenham HotSpurs, Chelsea leo wamewafuta machozi mashabiki wao kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Watford na sasa Chelsea wamefuzu kwa mzunguko wa nne wa kombe la FA.

Pamoja na ushindi huo, bado Chelsea hawakuonekana kucheza vizuri huku takwimu za mchezo huo kwa mujibu wa bbc Sports, walimiliki mpira kwa asilimia 51 dhidi ya 49 za Watford huku wakipiga mashuti 16 na kati ya hayo, sita tu ndiyo yaliweza kulenge lango.

Baada ya dakika 45 kumalizika bila timu hizo kufungana, kocha wa Chelsea Jose Mourinho aliamua kuwaingiza Diego Costa na Willian ili kuongeza nguvu na hapo ndipo uhai wa Chelsea ulipoongezeka. 

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Willian, Loic Remy na Kurt Zouma aliyefunga bao la tatu. Mourinho alifanya mabadiliko ya wachezaji wanane kutoka kikosi kilichofungwa na Spurs na hivyo isingekuwa rahisi kwa timu hiyo kucheza kwa kiwango cha juu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!