Lukas Podolski kuwavaa Juventus
Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani, Lukas Podolski amefanikiwa kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kutoka klabu ya Asrenal na kujiunga vijana wa Roberto Mancini baada ya dirisha la usajili nchini Italia kufunguliwa siku ya Jumatatu.
Inter Milan imethibitisha kuwa imeshakamilisha kila kitu na mchezaji huyo ambaye ataichezea timu hiyo katika kipindi chote kilichobakia msimu huu,Podolski alikuwepo katika jiji la Milan tangu wiki iliyopita ili kukamilisha usajili huo.
Sasa Podolski anaweza kucheza katika mechi dhidi ya Juventus siku ya Jumatano endapo atapangwa na kocha wa timu hiyo Roberto Mancini.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefunga magoli 47 katika michezo 121 aliyoichezea timu ya taifa ya Ujerumani hadi sasa.
Podolski amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Arsenal msimu huu kwani ameshindwa kufunga goli lolote katika michezo sita aliyoichezea timu hiyo katika ligi kuu nchini Uingereza msimu huu.
Podolski amefanikiwa kufunga magoli 31 katika michezo 82 alizoichezea timu ya Arsenal katika mashindano mbalimbali tangu alipojiunga na timu hiyo msimu wa 2012-2013 akitokea klabu ya Fc Cologne ya nchini Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment