Siku za Joseph Owino zinahesabika.
Na Florence George
Beki wa kati wa klabu ya Simba Joseph Owino anadaiwa kuanza kusaka maisha mapya baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu na viongozi hawaonyeshi nia ya kumpatia mkataba mpya huku nafasi yake ikitajwa kuja kuzibwa na Raphael Kiongera, .
Mkataba wa beki huyo umebakiza miezi sita na baada ya usajili wa Juuko Mursheed kutoka Uganda, Owino ameonekana kupoteza namba na hiyo ni dalili kuwa maisha yake msimbazi siku zinahesabika.
Mursheed na Hassan Isihaka kwa sasa ndiyo wanaocheza kama walinzi wa kati na hii ni ishara mbaya kwa beki huyo raia wa Uganda. Leo Simba atashuka dimbani kucheza na timu ya Jang'ombe mchezo wa robo fainali ya Mapinduzi Cup.
Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuwa beki huyo anamatatizo ya kifamilia na ndiyo sababu iliyofanya asiambatane na timu kuelekea Zanzibar, kuna habari nyingine zimetoka leo zikieleza kuwa beki huyo anaonekana hana furaha kwenye kikosi hicho na huko Kenya hakwenda kwa sababu za kifamilia.
0 comments:
Post a Comment