Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 January 2015
Thursday, January 08, 2015

Juma Kasseja amalizana na Yanga.


 Na John Oscar

Kipa Juma Kasseja hatimaye "ndoa" yake na klabu ya Yanga imefikia tamati baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano na kuamua kuvunja mkataba. 

Kasseja ambaye alisajiliwa na Yanga kwa ada ya Milioni 40 baada ya kutemwa na Simba, amekuwa kwenye mgogoro wa chini kwa chini na Yanga kwa muda mrefu kutokana na madai mbalimbali.

Wakati Yanga wanamsajili ilidaiwa kuwa kipa hiyo alilipwa pesa nusu huku kiasi kilichobakia akipewa ahadi ya kumaliziwa. Kasseja kwa miezi ya hivi karibuni amekuwa akisikika akilalamika juu ya kutopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku kukiwa pia na  madai ya kutomaliziwa Milioni 20 ambazo ni sehemu ya fedha za usajili wake.

Kwa muda wote ambao Kasseja amekaa na Yanga ameweza kudakia timu hiyo mechi 15 tu na katika michezo hiyo, mechi tano zilikuwa za ligi kuu na moja ya klabu bingwa Afrika. 

Wakati Yanga wanamsajili kipa huyo, lengo ilikuwa ni kuja kumtumia kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kutokana na uzoefu wake lakini malengo hayo hayakutimia kufuatia timu hiyo kuondoshwa mapema kabla hata ya hatua ya makundi.

Kasseja aliendelea kuwa kwenye hali ngumu kutokana na makocha wanaokuja Yanga, kumtumia Deogratius Munishi kama kipa namba moja huku Kasseja akiwa chaguo la pili na Ally Mustapha akibakia kama kipa namba tatu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!