Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 January 2015
Monday, January 12, 2015

Goli bora ni la James Rodriguez.


Na Chikoti Cico

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Colombia na klabu ya Real Madrid James Rodriguez amenyakua tuzo ya goli bora la mwaka la FIFA maarufu kama “Puskas award” kwa mwaka 2014.

James ambaye alifunga goli hilo kwa shuti kali la yadi 25 katika mchezo dhidi ya Uruguay kwenye fainali za kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazili, amechukua tuzo hiyo mbele ya magoli yaliyofungwa na Stephanie Roche kutoka Jamhuri ya Ireland na Robin van Persie kutoka Uholanzi.

Kiungo huyo mshambuliaji ambaye alihudhuria hafla ya utoaji wa tuzo hizo nchini Uswisi akiwa na mkewe Daniela Ospian pia aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo ya kombe la Dunia huku akifunga jumla ya magoli sita na kuiwezesha Colombia kufika mpaka robo fainali ya michuano hiyo mikubwa duniani kabla ya kutolewa na Brazili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!