Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 January 2015
Tuesday, January 13, 2015

Mshambuliaji wa Arsenal atua Crystal Palace.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya Arsenal Mfaransa, Yaya Sanogo amesajiliwa kwa mkopo na klabu ya Crystal Palace mpaka mwisho wa msimu huu wa ligi kuu ya nchini Uingereza huku akiwa ameichezea Arsenal michezo sita tu toka msimu huu uanze na kuifungia klabu hiyo toka jijini London goli moja tu.

Sanogo ambaye pia alitakiwa na klabu za Bordeaux, Hull Cuty na Qeens Park Rangers anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Crystal Palace Alan Pardew ambaye amehamia klabuni hapo akitokea timu ya Newcastle United.

Kocha huyo wa Palace akimwongelea Sanogo kwenye mtandao wa klabu hiyo alisema “ni mchezaji kijana ambaye mwenye matarajio makubwa, mtu ambaye nimekuwa nikimfwatilia binafsi na pia klabu hii hivyo hilo limekaa sawa.

Tumempa nafasi, anahitaji kucheza michezo zaidi na nadhani yuko tayari kwa hilo na amethibitisha hilo Arsenal. Ni ngumu kupata nafasi kwenye timu yao lakini anakaribia kuanza na sisi”.

Naye Sanogo akiongea baada ya kukamilisha usajili huo alisema “wakati Meneja wa Arsenal alipoongea na mimi kuhusu Crystal Palace nilikuwa na furaha sana kwasababu nataka kucheza mechi zaidi.

Akiendelea kuzungumza, Sanogo amesema, "nadhani Palace ni timu nzuri, niliangalia mchezo dhidi ya Totteham na ulikuwa mchezo mzuri kutoka kwa wachezaji, natumai nitaisaidia klabu kuwa na mafanikio ya nusu ya pili ya msimu”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!