Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 January 2015
Monday, January 12, 2015

La liga yatisha timu bora ya FIFA.


Na Chikoti Cico

Ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama La liga” imetisha baada ya kutoa wachezaji wengi kwenye timu bora ya wachezaji 11 wa FIFA kwa mwaka 2014. La liga imetoa wachezaji watano katia ya 11 katika kikosi hicho kinachojulikana kama “2014FIFPro World XI team”.

Wachezaji kutoka La liga ni Christiano Ronaldo (Real Madrid), Lionel Messi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid) na Toni Kroos (Real Madrid), ingawa Toni Kroos amechaguliwa huku sehemu kubwa ikiwa ni wakati akiichezea klabu ya Bayern Munich kabla ya kuhamia Real Madrid mwezi Agasti mwaka jana.

Ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga inashika nafasi ya pili kwa kutoa wachezaji wa tatu kwenye kikosi hicho bora cha FIFA huku wachezaji wote hao wakitoka klabu ya Bayern Munich ambao ni Manuel Neuer, Philipp Lahm na Arjen Robben.

Nayo ligi kuu ya nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 imetoa wachezaji wawili ambao ni mabeki David Luiz na Thiago Silva wote wakiichezea klabu ya PSG ingawa Luiz alihama toka Chelsea kwenda PSG kwenye majira ya joto mwaka jana.

Ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu kama Barclays Premier League yenyewe imetoa mchezaji mmoja tu ambaye ni Angel Di Maria anaichezea klabu ya Manchester United ingawa amechaguliwa kwenye kikosi hicho baada ya kuonyesha huku sehemu kubwa ikiwa ni wakati akiichezea Real Madrid kabla ya kuhamia klabu ya Man United mwezi Agasti mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!