Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 January 2015
Thursday, January 15, 2015

Dili la Chelsea lasimama.



Na Chikoti Cico

Dili la pauni milioni 25 la udhamini wa jezi za Chelsea kutoka Turkish Airlines ambalo lilitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana linaelekea kubuma baada ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili kusimama.

Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema kampuni hiyo ambayo ina mkataba binafsi na mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba bado imelibakisha swala hilo kwenye meza ya mazungumzo kutokana na malipo ya udhamini huo kuonekana ni makubwa sana.

Udhamini huo wa pauni milioni 25 kama utakamilika utaifanya Chelsea kuwa nafasi ya pili nyuma ya Manchester United na juu ya Liverpool na Arsenal kwenye udhamini wa jezi ndani ya ligi kuu nchini Uingereza.

Pamoja na mazungumzo hayo na Turkish Airlines kusimama klabu ya Chelsea bado inaendelea na mazungumzo na kampuni zingine huku mmiliki wa klabu hiyo Mrusi Roman Abramovich akitaka klabu hiyo kuwa namba moja kwenye mambo ya biashara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!