Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 July 2013
Saturday, July 13, 2013

NIONAVYO MIMI SIONI TATIZO KWA ALCANTARA KWENDA BAVARIANS.



Mashabiki wa united wengi wamekosa raha baada ya kusikia Pep Gaudiola anataka kumsajili kiungo wake wa zamani Thiago Alcantara toka FC Barcelona.

Binafsi namuona Alcantara kama star anayechipukia na bado angehitaji pengine muda kuweza kuonyesha uwezo wake.Nafasi yake kwa sasa pale united inachezwa na Shinji Kagawa,kama united watampata itakuwa nzuri na wakimkosa sioni, kama wanatakiwa kuwa wanyonge.

Sasa kama kwa Alcantara tu mnakuwa wanyonge hivyo,je mngekuwa mnakaribia kumnasa mmoja kati ya Mario Gotze,Fabregas,carzola au Mata simngeweka kabisa msiba?

United bado inaweza kupata ubingwa na kikosi hiki hiki cha kimagumashi.

Alcantara bado sio mchezaji tegemeo wa kubadili matokeo kama Iniesta,Messi,CR7,Neymar na RVP.man u fans,muwe na amani tu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!