Na Chikoti Cico
Kiungo wa Fiorentina Mcolombia Juan Cuadrado anakaribia kutua klabu ya Chelsea wakati dirisha dogo la usajili likikaribia ukingoni katika usajili ambao utaigharimu klabu hiyo kiasi cha pauni milioni 26.8.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anataka kukamilisha dili hilo kabla ya Jumatatu ambapo ndiyo mwisho wa dirisha dogo la usajili huku kocha huyo pia akitaka akitamani kukamilisha usajili wa Coudrado kabla ya mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester City hapo Jumamosi.
Fedha kwaajili ya usajili wa Coudrado zinatarajiwa kutokea kwenye dili lingine la klabu ya Chelsea ambao wanatarajia kumuuza Andre Schurrle kwa klabu ya Wolfsburg ya nchini ujerumani kwa ada ya kiasi cha pauni milioni 27.
0 comments:
Post a Comment