Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 January 2015
Friday, January 30, 2015

Schurrler kutua Wolfsburg.


Na Chikoti Cico

Winga wa klabu ya Chelsea Andre Schurrle anakaribia kutua klabu ya Wolfsburg inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga na tayari ameshakubaliana na klabu hiyo mambo binafsi huku akisubiria Chelsea wakubali ada ya uhamisho.
Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema Schurrle mwenye umri wa miaka 24 anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya siku ya Ijumaa (leo) nchini Ujerumani wakati dili hilo likikaribia kukamilika.
Klabu ya Wolfsburg imetoa ofa ya pauni milioni 21 na ukichanganya na mambo mengine ofa hiyo inaweza kufikia pauni milioni 27 ingawa klabu ya Chelsea inahisi kwamba ofa hiyo ni ndogo tofauti na matarajio yao.
Schurrle ambaye alijiunga na klabu ya Chelsea akitokea klabu ya Bayern Leverkusen kwa ada ya kiasi cha pauni milioni 18 ameamua kuondoka kwenye klabu ya Chelsea baada ya kuwa na nafasi ndogo ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jose Mourinho huku mpaka sasa akiwa ameanza kwenye michezo mitano kati ya 22 ya ligi kuu nchini Uingereza.
Wakati huo huo klabu ya Wolfsburg imempeleka kwa mkopo mshambuliaji wake mwenye umri wa miaka 35 Ivica Olic ambaye ni moja ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi klabuni hapo ili kutoa nafasi kwaajili ya malipo ya dili la Schurrle.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!