Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa timu ya Chelsea, Diego Costa anaweza kuukosa mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City utakaopigwa siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Costa ameshtakiwa na shirikisho la soka la nchini Uingereza (FA) kwa kukosa la kumkanyaga kiungo wa Liverpool Emre Can kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Capital One uliochezwa usiku wa Jumanne ambapo Chelsea waliibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuingia fainali.
FA wamemshtaki Costa ikiwa ni mojawapo ya hatua kuhusiana na kumkanyaga Can lakini hawatachukua hatua zozote dhidi ya Martin Skrtel ambaye alipambana na Costa kwenye mchezo huo.
Costa aliepuka adhabu kwenye mchezo huo dhidi ya Liverpool baada ya mwamuzi Michael Oliver kushindwa kuona tukio hilo huku kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akidai tukio hilo lilikuwa ni bahati mbaya na kama Costa akikataa shtaka hilo, kamati ya watu wa tatu wa FA itapitia ushahidi na kutoa uamuzi kabla ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Manchester City.
Taarifa ya FA inasomeka “shtaka ni kuhusiana na tukio lilimhusiha mshambuliaji wa Chelsea dhidi ya Emre Can wa Liverpool ambalo lilitokea kwenye dakika ya 12 ya nusu fainali ya pili ya kombe la Capital One kwenye uwanjwa wa Stamford Bridge usiku uliopita (Jumanne 27 Januari 2015). Mchezaji ana mpaka saa 12jioni siku ya Alhamisi tarehe 29 Januari 2015 kujibu shtaka hilo”.
Kiungo wa Stoke City City Charlie Adam alifungiwa michezo mitatu siku nne baada ya kumkanyaga Olivier Giroud wa Arsenal, Sascha Riether wa Fulham alipewa adhabu kama hiyo baada ya kusimama juu ya mguu wa Adanan Januzaj kwenye msimu uliopota mwezi Novemba.
0 comments:
Post a Comment