Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Henry ambaye kwasasa ameajiriwa kama mchambuzi wa soka kwenye kituo cha televisheni cha Skysports ameanza mafunzo ya ukocha baada ya kuamua kustaafu soka mwishoni mwa mwaka uliopita.
Henry ametajwa kuanza kuchukua kozi za ukocha kutoka shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) nchini Wales, mshambuliaji huyo ambaye aliwahi pia kuichezea klabu ya Barcelona ametajwa kufanya kozi ya ukocha kwa leseni ya ngazi B ya UEFA.
Henry alifanya uwasilishaji kwenye kikosi cha Wales umri chini ya miaka 16 mapema wiki hii na anatarajiwa kuungana na mchezaji mwenzake wa Arsenal Freddie Ljungberg katika kuchukua kozi hiyo ya ukocha.
Pia taarifa zinasema Henry mwenye umri wa miaka 37 kama akifaulu inawezekana akakamilisha leseni ya ngazi A kwenye majira ya joto mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment