Bent kutimka Aston Villa
Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na Aston Villa ,Darren Bent atajiunga kwa mkopo na timu ya ligi daraja la kwanza Nchini Uingereza klabu ya Derby County kwa kipindi chote kilichobaki msimu huu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Aston Villa siku ya ijumaa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ni mmoja kati wa wachezaji 24 ambao wamefunga magoli zaidi ya 100 katika ligi kuu nchini humo,alikuwa anacheza kwa mkopo katika timu ya Brighton na Hove Albion mwezi uliopita.
Bent ambaye ameichezea timu ya taifa ya Uingereza mara 13 tangu mwaka 2006 hadi 2011,alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Ipswich Town klaba ya kutimkia Charlton Athletic, Tottenham Hotspur na Sunderland.
Mchezaji huyo alijiunga na Aston Villa akitokea klabu ya Sunderland kwa dau lililoweka rekodi katika timu hiyo la kiasi cha Euro Millioni 18 mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment