Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

Gerrard huyooo Marekani


Na Chikoti Cico

Baada ya nahodha na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard kutangaza kwamba mwishoni mwa msimu huu ataondoka kwenye timu hiyo, taarifa kutoka nchini Marekani zinasema Gerrard anakaribia kujiunga na klabu ya LA Galaxy.

Gerrard ambaye ameichezea Liverpool kwa miaka 26 kabla hajatangaza kuamua kuachana na timu hiyo mwisho wa msimu anatarajia kuingia mkataba wa miezi 18 na klabu hiyo ya nchini Marekani kwa dili la pauni milioni 3.9.

Wakati Gerrard bado ana miezi sita ya kuichezea Liverpool inaeleweka kwamba mazungumzo kati yake na LA Galaxy yanaendelea na kama wakifikia muafaka basi kiungo huyo mahiri wa Uingereza atajiunga na klabu hiyo mapema mwezi wa saba.

Gerrard alifikia uamuzi wa kuachana na Liverpool miwshoni mwa msimu huu baada ya kufanya mazungumzo na kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers ambaye alimweleza wazi kwamba katika msimu unaokuja atakuwa na nafasi ndogo ya kupangwa mara kwa mara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!