Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na Manchester City, Sergio Kun Aguero anatarajiwa kurudi uwanjani katika mechi dhidi ya Arsenal January 18, hii ni kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini.
Kocha huyo anaamini kuwa Aguero ambaye hadi sasa ameshafunga magoli 19 atarejea uwanjani siku hiyo dhidi ya vijana wa Arsene Wenger kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu .
Pia kocha huyo anaamini kuwa Mshambuliaji wa kimataifa wa Bosnia, Edin Dzeko atarudi uwanjani hivi karibuni kuelekea mchezo wao dhidi ya Everton January 10.
Dzeko ambaye amekosekana katika michezo mitano ya hivi karibuni anasumbuliwa na majeruhi ambayo aliyapata walipokuwa wakipasha misuli joto katika mechi dhidi ya Leicester,wakati Aguero aliumia katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Everton mwanzoni mwa mwezi December mwaka jana.
Pellegrini anaamini kuwa washambuliaji hao watakuwepo katika mchezo dhidi ya timu ya Chelsea January 31 ambao ndio wanaofukuzana kwa karibu katika mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwani hadi sasa timu hizo zimeshacheza michezo 20 huku kila moja ikiwa na pointi 46.
0 comments:
Post a Comment