Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 January 2015
Friday, January 02, 2015

Kumbe Phiri alikuwa anadai mishahara miezi mitatu?



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuiongoza klabu ya Simba kwenye mechi nane huku timu ikipata ushindi mara moja, kutoka sare mara sita na kuchezea kichapo mara moja, kocha Patrick Phiri ametemwa na klabu ya Simba huku taarifa zikibainisha kuwa bado anaidai klabu hiyo mishahara ya miezi mitatu.

Akizungumza na kituo cha Redio cha E-FM msemaji wa timu hiyo Hamphrey Nyansio, amethibitisha kuwa tayari uongozi huo umeachana na kocha huyo na taratibu zote za kuvunja mkataba zimefanyika. 

Nyansio amethibitisha kuwa tayari kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar kimefanya mazoezi leo chini ya kocha mpya, Goran Kuponovic.

Kuhusu madai ya Dolla elfu 12 anazodai Phiri ambazo ni mishahara ya miezi mitatu, Nyansio amesema kocha huyo atapewa kila shahiki yake. 

Imebainika kuwa kocha huyo alikuwa analipwa Dolla elfu nne tu kwa mwezi na huyu anaweza kuwa kocha wa kigeni kuwahi kulipwa mshahara kiduchi sana kwenye ligi kuu Tanzania bara kwa siku za hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!