Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 December 2014
Wednesday, December 24, 2014

Zlatan ageuka mbogo!


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden na klabu ya PSG, Zlatan Ibrahimovic akasirishwa kuibuka wa pili kwenye tuzo za mwanamichezo bora wa muda wote nchini Sweden zilizotolewa na gazeti la Dagens Nyheter.

Wasomaji wa gazeti hilo maarufu nchini Sweden walimpigia kura nyingi mchezaji bora wa tenisi wa nchi hiyo Bjorn Borg ambaye ndiye aliibuka mshindi wa kwanza, Borg ambaye ni bingwa mara tano kwenye michuano ya Wimbledon alishika nafasi ya kwanza huku Zlatan akishika nafasi ya pili na mchezaji mwingine wa tenisi Jan-Ove Walder akiibuka wa tatu.

Baada ya kupongezwa na gazeti ka Dagens Nyheter, Zlatan hakuonekana kufurahishwa kuibuka mshindi wa pili na wakati anahojiwa alisema “Asante lakini kumaliza wa pili ni kama kumaliza wa mwisho, katika orodha hiyo nigekuwa namba 1,2,3,4 na 5, nikiwaheshimu wengine”

Lakini pamoja na kuonyeshwa kutokufurahishwa na nafasi hiyo ya pili kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya gazeti hilo, Zlatan bado alionyesha kumkubali mshindi wa tuzo hiyo Borg kwa kusema “ni mtu mzuri na ni gwiji anayeishi”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!