Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 December 2014
Wednesday, December 24, 2014

Xavi amnyima Ronaldo Ballon d’Or.


Na Chikoti Cico

Nahodha wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez azungumzia kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or na kumwondoa kabisa Christiano Ronaldo kwenye kinya’nganyiro hicho.

Xavi anaamini mfungaji huyo bora wa la liga kwa msimu uliopita hastahili kabisa kuwepo kwakuwa hakufanya lolote kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazili mapema mwezi Julai mwaka huu.

Kwenye mahojiano na gazeti la Sport Xavi ambaye anasifika kwa upigani bora wa pasi aliulizwa kama angekuwa nahodha wa Hispania angempigia nani kura? na Xavi alijibu “Wakwanza Leo (Lionel Messi), wapili (Philipp) Lahm na watatu (Javier) Mascherano.

Na alipoambiwa kwamba mchezaji mwenzake wa Barcelona Neymar alimweka Ronaldo kwenye orodha yake ya washindi wa tuzo hiyo na kumwondoa Lahm,.

Xavi alijibu kwamba “ ni kwamba, Christiano hakufanya kitu kwenye kombe la Dunia na nafikiri katika mwaka wa kombe la Dunia hicho kinaelezea zaidi msimu”

Kwenye kinyag’anyiro cha kuwania tuzo hiyo ya heshima itakayotolewa mwezi wa kwanza mwaka 2015 mpaka sasa wamebaki Ronaldo, Messi na Neuer katika orodha ya washindi huku Ronaldo akipewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi wa tuzu hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!