Na Chikoti Cico
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameonyesha kutokuwa tayari kuifundisha timu yake taifa ya Ureno hata kama akipewa nafasi na shirikisho la soka la nchini humo (FPF).
Mourinho amezungumza hayo wakati akihojiwa na Clare Blading kwenye kipindi maalumu cha BT Sport kitakachorushwa siku ya tarehe 26 Desemba.
Mourinho ambaye amezifundisha klabu mbalimbali kwa mafanikio makubwa alipoulizwa kama atapenda kuifundisha timu ya taifa lake alisema “Hapana, walijaribu kunichukua mara nyingi na ilikuwa mara moja tu nilikubali kwasababu ilikuwa kazi ya masaa machache”
“Nilitaka kufanya kwa wakati mmoja klabu na timu ya taifa, na wakati huo nilitaka kukubali lakini Raisi wangu kwa wakati huo aliamua kutokiruhusu kufanya kazi ya timu ya taifa”
Aliendelea kusema “ baada ya hapo niliwaza na nakubali haikuwezekana kufanya kazi zote kwa muda huo huo, hata sio maadili kwa meneja kuwa na kazi mbili huku kukiwa na meneja wengi wasio na kazi, haikubaliki”
Pia mourinho aliwahi kuhusishwa kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza na anakubali kwamba alikuwa sawa kuukubali ushauri wa mke wake (Matilde) wa kutokukubali kazi hiyo kwasababu ya kupenda kazi za kila siku za klabu.
Jose akiongelea hilo alisema “alikuwa sahihi, ni mapema sana kwangu. Napenda siku baada ya siku, napenda presha ya siku baada ya siku, mafunzo, kusafiri, mechi, ushindani”.
“Nakumbuka sawa kabisa kuna muda mechi iliyofwata ya Uingereza ilikuwa ni Paris, Ufaransa v England, mechi ya kirafiki. Na nilikuwa tayari nafikiria nani wa kuwachagua, nani wa kucheza, jinsi ganiu nifanye, alikuja kwangu (Matilde) na kusema “mechi inayofwata ni lini?”
“Ah mechi inayofwata ni ndani ya miezi miwili”. “nini utafanya kwa miezi miwili, nini unafanya, nini unafikiria?’ alikuwa anasema. “Sahau, sio kwaajili yako, labda kwa miaka 20”
0 comments:
Post a Comment