Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 December 2014
Thursday, December 25, 2014

Walcott ni noma!!


Na Chikoti Cico
 
Pamoja na kuwa ligi ya Uingereza imetawaliwa na ratiba ngumu ya mechi za mfululizo kwenye kipindi cha sikukuu za mwisho mwaka lakini bado kuna wachezaji wameonyesha kuwa bora kwa kuzifumania nyavu hasa siku ya tarehe 26 Desemba maarufu kama “boxing day”.

Katika historia ya ligi kuu nchini Uingereza hasa kwa wachezaji ambao wameshastaafu kucheza soka Robby Fowler ndiye anaongoza kwa kuzifumania nyavu siku ya “boxing day” huku akiwa amefunga magoli nane akizichezea timu za Liverpool na Manchester City kati ya mwaka 1994-2004.

Pia Thierry Henry and Robbie Keane nao walikuwa vinara wa kufunga magoli kwenye mechi zinachezwa siku ya tarehe 26 Desemba huku kila mmoja akifunga magoli saba katika mechi walizocheza.

Na kati ya wachezaji ambao bado hawajastaafu na ambao ni vinara wa kufunga magoli siku ya tarehe 26 Desemba ambaye anaongoza kwenye orodha hiyo ni winga wa Arsenal Theo Walcott akiwa amezifumania nyavu mara sita huku akifuatiwa kwa karibu kabisa na Gareth Barry ambaye nae amezifumania nyavu mara nne huku akifunga mara tatu akiichezea Aston Villa na mara moja akiwa na Manchester City.

Hivyo kuelekea michezo ya “boxing day” kwa mwaka 2014 inawezekana Walcott wa Arsenal na Barry ambaye kwasasa anaichezea Everton wakaendelea kuwapa mashabiki wa timu zao zawadi za Krismasi huku timu zao zikiendelea kung’ara kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!